Back to top

Serikali yaidhinisha matumizi ya aina mpya 40 za mbegu.

05 January 2020
Share

Serikali imeidhinisha matumizi ya aina 40 mpya za mbegu za mazao kwa ajili ya msimu wa kilimo 2019/2020 huku Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisema mbegu hizo zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa na sifa ikiwemo kutoa mavuno mengi, kuhimili magonjwa kukomaa ndani ya muda mfupi pamoja na kupendwa na wakulima na walaji.

Akitangaza kuidhinishwa kwa matumizi ya mbegu hizo ambazo ni za mahindi, mpunga, alizeti, muhogo, mtama, ulezi ,viazi vitamu na pamba Mhe Waziri Hasunga anasema uamuzi huo umetokana na ushauri kutoka kamati ya taifa ya mbegu kwa kuzingatia sheria kanuni namiongozo ya uzalishaji mbegu.