Back to top

Serikali yakarabati Makumbusho ya Kawawa wilayani Songea

09 August 2018
Share

Serikali inakarabati Makumbusho ya Rashid Mfaume Kawawa kuenzi mchango wake ambapo jumla ya shilingi milioni 170 zinatumika kukarabati Makumbusho hayo yaliyoko Bombambili wilayani Songea mkoani Ruvuma.
  
Makumbusho  hayo yanakarabatiwa na wakala wa majengo nchini(TBA)ambapo kaimu meneja wa TBA  mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mtapuli Juma  amewaeleza viongozi wa mkoa wa Ruvuma waliotembelea Makumbusho  hayo kuwa ukarabati wake unahusisha ukarabati wa nyumba  na pia kuweka uzio na kufanya Makumbusho hiyo kuwa na mwonekano wa kuvutia.

Mhifadhi kiongozi wa Makumbusho ya Majimaji Bw.Baltazari Nyamusya anasema kuwa Makumbusho hiyo inakuwa  ya pili wilayani Songea ikiwa na vitu mbalimbali vilivyotumika na  marehemu Rashid Kawawa pia ikiwa na ukumbi wa chini ya ardhi ambao aliutumia na wenzake kupanga harakati za ukombozi.
 
Hivi karibuni naibu waziri wa maliasili na utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga  alipozitembelea Makumbusho  hayo alisema Makumbusho  ya   Majimaji  na  ya Kawawa yanawakumbusha watanzania uzalendo.

 

 

 

.