Back to top

Serikali yakataa mgodi wa Williamson Diamond kuuzwa.

05 July 2020
Share

Waziri wa Madini Dotto Biteko amekataa mpango wa uongozi wa mgodi wa madini ya Almasi wa Williamson Diamond Shinyanga kuuza mgodi huo kwa madai kuwa uzalishaji umeshuka huku akiagiza wafanyakazi wote wa mgodi huo waliopewa likizo kwa kulipwa nusu mshahara warudishwe kazin mara moja kuendelea na kazi na kulipwa stahiki zao kama kawaida.

 


Waziri Biteko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo,viongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga na wawakilishi wa wafanyakazi wa mgodi wa Williamson Diamond.