Serikali imesema itachukua hatua kali kwa watu wanaokaidi amri ya kuwataka kutokujenga na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye mapito ya wanyamapori (ushoroba) kwa kuwa wanachangia kufifisha juhudi za wadau wa uhifadhi na kusababisha migogoro inayoendelea kushamiri kati ya binadamu na wanyamapori .
Akizungumza na wadau wa uhifadhi mkoani Manyara,naibu waziri wa maliasili na utalii Constantini Kanyasu amesema kuwa wanaojenga kiholela katika maeneo ya ushoroba hawatalipwa fidia na badala ake watachukuliwa hatua.
Mkurugenzi wa wanyamapori kutoka wizara ya maliasili na utalii , Dkt.Maurusu Msuha amesema kuwa uanishwaji ,upimaji na uwekaji wa mipaka ya maeneo ya ushoroba unapaswa kuwashirikisha wananchi ili kuepuka migogoro isiyokua ya lazima.
Katibu wa jumuiya ya hifadhi ya jamii Burunge Bw.Benson Mwaise na mkuu wa wilaya ya Babati Bi.Elizabeth Kitundu wamesema kuwa elimu kwa wananchi inahitajika ili kufanikiwa kulinda ushoroba.