Back to top

Serikali yapiga marufuku maafisa ardhi kupima maeneo kwa upendeleo.

12 October 2018
Share

Serikali imepiga marufuku maafisa wa idara ya ardhi nchini kuacha kuwapora ardhi wananchi wasio na uwezo wakati wa zoezi la upimaji maeneo kwa ajili ya urasimishaji badala yake imeagiza wananchi wanaoishi katika viwanja hivyo wapewe kipaumbele cha kwanza cha umiliki kabla ya kupewa mmiliki mwingine ili kuondoa migogoro ya mara kwa mara.
 
Agizo hilo limetolewa mjini Musoma mkoani Mara na naibu waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Dkt Angelina Mabula, wakati akizungumza na watumishi wa idara ya ardhi,viongozi wa wilaya na watendaji wakuu wa halmashauri za Musoma vijijini,Butimama na halmashauri ya manispaa ya Musoma.
 
Naye mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano,akizungumza katika mkutano huo,amesema kuwa baadhi ya maafisa wa idara kwa kukosa uadilifu, wamekuwa wakipima viwanja kwa kuchonganisha watu, hatua ambayo amesema imekuwa ikichangia migogoro mikubwa wilayani humo.