Back to top

Serikali yapiga marufuku ugawaji viwanja 'pandikizi' .

16 October 2018
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt. Angeline Mabula amepiga marufuku ugawaji viwanja ambavyo tayari vimemilikishwa huku mmiliki wake wa awali akitafutiwa eneo lingine.
 
Hatua hiyo inafuatia kushamiri kwa  tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri nchini kugawa maeneo ambayo tayari yana wamiliki wake wa awali na kuwapa watu wengine wenye uwezo kifedha huku wamiliki halali kuahidiwa kupatiwa kiwanja kingine.
 
Mhe. Mabula alitoa kauli hiyo wilayani Musoma mkoa wa Mara alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika Manispaa ya Musoma pamoja na halmashauri za wilaya za Musoma na Butiama wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya februari mwaka 2018.