Back to top

Serikali yaridhia idadi ya wachezaji wakigeni kubaki 10.

10 August 2020
Share

DAR ES SALAAM.

Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt.Harison Mwakyembe ametangaza uamuzi wa Serikali kuendelea kuruhusu idadi ya wachezaji 10 wakigeni.

Kadhalika idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuanza kucheza itabaki chini ya Baraza la Michezo BMT .

Akitangaza uamuzi huo leo Dkt.Mwakyembe ambaye ni miongoni mwa Mawaziri wasomi amesema Serikali imezingatia maoni ya wadau .

Pia amesema bado wizara kwakushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kitako kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa nankuingia Nchini.

" Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata wa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tu" Alisema Mwakyembe.

"Ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka Nje wawe na weledi, wawe na uwezo mkubwa"

Amesema kati watu 977 waliyotoa maoni, watu 809 wametaka idadi ya wachezaji 10 wakigeni.

Kando na hayo Wizara imeagiza watu wanaoajiriwa nchini wawe na ulazima wa kujifunza / kufunzwa lugha ya Kiswahili.