Back to top

Serikali yasema hakuna EBOLA nchini.

22 May 2018
Share

Naibu waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile amesema mpaka sasa hakuna taarifa za uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini huku akibainisha kuwa taifa limeimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani hasa kwenye mikoa ya jirani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo maradhi hayo yameripotiwa kuwepo.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na  ITV mjini Dodoma naibu waziri Dkt. Ndugulile amesema hakuna taarifa za uwepo wa maambukizi ya ugonjwa huo nchini na serikali imejipanga kuhakikisha inakabiliana na tishio la kuingia kwa Ebola nchini.

Katika hatua nyingine naibu waziri huyo amewataka wananchi kutoa taarifa mara watakapoona kuna mtu mwenye dalili za ugonjwa huo ambazo ni pamoja na kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.