Back to top

Serikali yasema itaendelea kutoza tozo kwa wanaovuka daraja la Kigambo

22 June 2018
Share

Serikali imesema itaendelea kutoza tozo kwa wanaovuka katika daraja la Kigamboni kutokana na kuwa sehemu ya  uwekezaji wa shirika la taifa hifadhi ya jamii NSSF ambalo linategemea mapato yanayopatikana katika daraja hilo katika kuendesha shughuli zake mbalimbali za shirika hilo ikiwemo kulipia mafao ya wanachama.

Hayo yamesemwa na naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde akijibu swali la Mhe. Zainab Mndolwa Amiri mbunge wa viti maalum aliyeuliza ni lini serikali itaacha kuwatoza wananchi  tozo ya kuvuka daraja hilo kama ilivyo kwa madaraja mengine nchini

Aidha Mhe.Mavunde amesema tayari serikali kupitia NSSF ambao ndio wanasimamia uendeshaji wa wa daraja hilo mpaka mwezi machi mwaka huu limeshakusanya kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 19 na milioni mia saba thalathini na nne tangu kuanza kutumika  rasmi kwa daraja hilo mwezi  May 2016

Amesema kwa sasa serikali iko mbioni kuweka utaratibu wa matumizi ya kadi maalum,mchakato ambao uko katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi wa kuweka mfumo huo wa malipo kwa wanaovuka darajani hapo ambao watakuwa na hiari ya kulipia kwa siku,wiki au mwezi kadiri ya uwezo wake