Back to top

Serikali yashauriwa kuweka mfumo wa kunusuru kilimo cha zao la Vanilla

17 January 2019
Share

Serikali imeshauriwa kuweka mfumo rasmi utakaonusuru kilimo cha zao la Vanilla mkoani Kagera kwa kudhibiti vitendo vya uvunaji wa Vanilla kwa njia ya wizi vinavyofanywa kwenye mashamba ya wakulima wa zao hilo nyakati za usiku na watu wasiojulikana ambao baadae uuza Vanilla hiyo kwa njia ya magendo kwa walanguzi toka nchi jirani. 

Ushauri huo umetolewa na Dkt.Mutayoba Bais mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na mtafiti kilimo na soko la mazao alipozungumza na ITV, amesema vitendo vya uvunaji wa Vanilla kwa njia wizi vinavyofanywa kwenye mashamba ya wakulima vinachangiwa na sababu ya kutokewepo kwa  mfumo rasmi wa kusimamia zao hilo ambalo kwa sasa lina thamani kubwa duniani. 

Kwa upande wake, meneja wa shirika la kuendeleza wakulima wa Vanilla Kagera (MAYAWA) Charles Kamando amesema katika msimu wa ununuzi wa Vanilla wa mwaka 2018/19 lengo lilikuwa ni kukusanya tani zaidi ya 60 za Vanilla mbichi lakini kutoka na vitendo vya wizi wa Vanilla lengo hilo halikufikiwa.