Back to top

Serikali yasitisha ubomoaji nyumba za wavamizi eneo la mnada wa Pugu.

13 September 2018
Share

Serikali imesitisha zoezi la kuwaondoa kwa nguvu na kubomoa nyumba 5,391 za wananchi zaidi ya elfu ishirini waliovamia na kujenga eneo la ekari 1,792 za mnada wa Pugu na kuwahakikishia kuwa watawamilikisha maeneo yao kwa kufuata taratibu za sheria.

Akitoa maamuzi ya serikali juu ya matokeo ya kamati ya wataalamu ya wizara yake na ya ardhi iliyoundwa awali tar 7/03 mwaka huu kuchunguza uvamizi katika eneo la mnada wa Pugu lenye ekari 1900 imebaini sehemu kubwa ya eneo imevamiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina amesema serikali itajenga mnada sehemu nyingine na ukikamilika mnada wa Pugu utahamishwa baadaye kwavile umevamiwa na ekari 108 zilizobakia hazitoshi.

Waziri Mpina aliambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi uongozi wa jiji la Dar es Salaam wataalamu wa wizara zote mbili serikali ya wilaya ya ilala ambapo Mh.Lukuvi aliwaambia wananchi wa mtaa Bangulo kuwa msamaha huo ni huruma ya Mh.Rais John Magufuli lakini lazma wananchi waondoe changamoto ya makazi holela kwa kupima maeneo yao kisheria.

Awali mkuu wa mkoa wa Dar es Dalaam Mh.Paul Makonda alitoa rai kwa wananchi kabla hawajanunua ardhi wajiridhishe ili kuepuka migogoro huku baadhi ya wananchi wakimshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali wananchi wanyonge.