Back to top

Serikali yatangaza neema kwa walimu waliopanda madaraja

15 April 2019
Share

Serikali imesema inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuwalipa walimu na watumishi wengine waliopanda madaraja na stahiki zao ambazo hawajapata kwa muda mrefu licha ya kupanda madaraja

Hayo yamesemwa bungeni Dodoma na naibu waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara akijibu swali lililoulizwa na baadhi ya wabunge la kwanini serikali haitoi malipo stahiki kwa walimu ambao wamewapandisha madaraja kwa mujibu wa taratibu

Mhe.Waitara amesema tayari serikali imeshatoa maelekezo kwa waajiri wote ikiwemo wakurugenzi wa mamlaka za serikali mitaa kuhuisha barua za kuwapandisha madaraja watumishi ikiwemo walimu  ili waanze  kulipwa malipo yao na kwamba serikali iliamua kusitisha kupandisha madaraja na malipo kutokana na kuhakiki vyeti vya watumishi ili kubaki na watumishi wenye sifa na wanaostahili