Back to top

Serikali yatoa ajira kwa walimu 2160 wa shule za sekondari.

20 August 2018
Share

Serikali imeajiri walimu 2160 wa shule za sekondari na kuagiza waajiriwa hao wapya kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ndani ya wiki mbili wakiwa na vyeti halisi vya taaluma na cheti cha kuzaliwa na watakaoshindwa kutimiza masharti hayo nafasi zao zitachukuliwa na kugawiwa kwa watu wengine wenye sifa.

Akizungumzia ajira hizo mpya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema walimu 1900 ni wa masomo ya sayansi na hisabati, 100 lugha ya fasihi katika kiingereza na 160 ni mafundi sanifu wa maabara ambao watasambazwa kwenye shule za sekondari 1721.

Waziri Jafo amewataka waajiriwa hao kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi na si makao makuu ya halmashauri ili kuomba uhamisho na yeyote atakayechukua posho ya kujikimu na kutokomea serikali itamchukulia hatua.

Watumishi hao wapya ni sehemu ya wahitimu 20101 waliotuma maombi ya ajira ofisi ya rais tamisemi june 17 mwaka huu.