Back to top

Seth aandika barua kwa DPP aomba msamaha.

10 October 2019
Share

Mshtakiwa katika kesi ya Uhujumu Uchumi, Habinder Seth ameandika barua ya kukiri na kuomba msamaha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) lakini hawajapa majibu.

Hayo yameelezwa Oktoba 10 na Wakili wake,Michael Ngalo Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shahidi wakati Kesi hiyo ilipotajwa.


Hata hivyo, Wakili Ngalo aliuomba upande wa mashtaka uweze kuwasaidia na kudai kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umechukua muda mrefu hivyo aliutaka upande wa mashtaka uwaahidi lini wanaukamilisha.


Baada ya Wakili Ngalo kueleza hayo, Wakili wa serikali Wankyo Simon alieleza kuwa ni kweli barua imepokelewa na inafanyiwa kazi majibu atapewa.


Kuhusu upelelezi,Wankyo alieleza kuwa bado haujakamilika na hawawezi kuahidi ni lini utakamilika .

Baada ya kusikilizwa Maelezo hayo ya pande zote, Hakimu Shahidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.