Back to top

Shahidi akwamisha Kesi ya Zitto Kisutu.

09 April 2019
Share

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imekwama kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe kutokana na shahidi wa upande wa mashtaka kuwa katika majukumu mengine ya kikazi.

Wakili wa serikali mkuu Tumaini Kweka ameiambia mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, mbele ya hakimu mkazi mkuu Huruma Shaidi kuwa shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi mahakamani hapo amepangiwa majukumu mengine na  wanaomba mahakama ipange tarehe kwa muda mfupi ujao ili waweze kuendelea na usikilizwaji.

Hakimu mkazi mkazi mkuu Mheshimiwa Huruma Shaidi amekubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 24 na 25 mwaka huu ambapo itakuja kwa ajili ya kusikilizwa.