Back to top

Shein aitaka SADC kuwa na mpango kazi wa kupambana na maafa.

21 February 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekit i wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa na mpango kazi na mikakati ya kupambana na maafa, hasa yale yanayotokea mara kwa mara katika ukanda huo.

Dkt.Shein  amesema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa siku nne wa nchi wanachama za SADC unaofanyika Zanzibar.

Dkt.Shein amesema fedha nyingi za maendeleo zinalazimika kwenda kwenye matukio ya maafa, hivyo hapana budi matatizo hayo ikiwemo ya  afya na kilimo yakawekewa mfuko maalum.

Mapema Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge, Mhe.Jenista Mhagama alitaja kazi ya kamati hiyo ya maafa ya SADC kuwa ni pamoja na kuyashauri mabaraza ya mawaziri.

Katibu Mtedaji wa SADC, Dkt.Stergomena Tax amesema nchi za SADC zimekumbwa na maafa makubwa, hivyo mkutano huo unatarajaiwa kutoka na mbinu za kujikinga.