Back to top

Sheria ya kudhibiti madini yasaidia kudhibiti utoroshaji madini.

22 February 2021
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.Samia Suluhu Hassan amesema utungaji wa sheria kali ya kudhibiti madini ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali madini inamnufaisha mtanzania na kukuza pato la taifa katika sekta hiyo ambayo inategemea kuchangia pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.
.
Akifungua kongamano la wadau wa madini Jijini Dar es salaam Mh.Samia amesema vitendo vya wizi wa madini kwa miaka mingi kabla ya kuwepo kwa sheria za kudhibiti wizi huo madini mengi yalikuwa yanasafirishwa nje ya nchi bila taifa kunufaika na rasilimali hiyo kama ilivyo kwa sasa.
.
Katika hotuba yake makamu wa rais amesema dhamira ya serikali ni kuhakjkisha sekta ya madini inaendelea kukua na kunufaisha wawekezaji ikiwemo kutatua changamoto  zinazowakabili wachimbaji wa madini. 
.
Pia Mh.Samia amesisitiza uchimbaji wenye kuleta maendeleo endelevu kwa kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yote ya uchimbaji ikiwemo kuepuka utirishaji wa maji yenye kemikali katika makazi ya watu na kufukia mashimo hatarishi.