Back to top

Sheria za uvuvi zilizopitwa na wakati kupitiwa upya.

16 April 2021
Share

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema inatarajia kupitia upya sera na sheria za uvuvi ambazo zimepitwa na wakati na kushindwa kumsaidia mvuvi ikiwemo kutenganisha uuzaji wa Sangara na Mabondo katika viwanda mbalimbali vya kuchakata samaki hapa nchini.

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalllah Ulega ameyama hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe.Neema Lugangira aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kubadilisha sera na sheria za uvuvi ambazo zimepitwa na wakati na kushindwa kumsaidia mvuvi kwa sasa kunufaika na mazoa yake ya uvuvi.

Mhe.Ulega amekiri kuwa soko la Mabondo kwa sasa lina soko kubwa hivyo mvuvi anapouza Sangara mzima katika viwanda akiwa na mabondo yake anapunjwa malipo yake hivyo kwa sasa serikali inangalia mfumo wa kubalidisha sheria za uuzaji na ununuzi wa samaki hapa nchini.