Back to top

Shule ya Kiislam ya Istiqama yateketea Moto Tabora

27 September 2020
Share

Wanafuzni 40 wa bweni katika shule ya msingi na sekondari ya Istiqama iliyopo katika manispaa ya Tabora, wamenusurika kifo baada ya mabweni waliyokuwa wamelala kuteketea kwa moto ambao haukujulikana chanzo.
 
Mhudumu wa watoto Bibi Mwanaidi Shabani amesema baada ya tukio hilo jambo la kwanza alilolifanya ni kuwakimbiza nje wanafunzi ili kuwanusuru katika tukio hilo ambapo hakuna madhara kwa watoto hao.
 
Mkuu wa kikosi cha Jeshi la Zimamoto na uokoaji manispaa ya Tabora mkaguzi Maganga Peter Mgombere, amesema kwa mda waliopata taarifa waliweza kufika eneo la shule hiyo na kuudhubiti moto ili usisambae katika mabweni jirani na hilo lililoteketea.
 
Shehe mkuu wa wilaya ya Tabora mjini na katibu wa Bakwata mkoa wa Tabora wamewataka wazazi na Watanzania kuwa na subira wakati uchunguzi ukifanywa na wahusika, kutokana na matukio hayo kuongezeka, yakigharimu rasilimali za miundombinu ya shule husika.