Back to top

Shule ya Sekondari yenye walimu wawili mkoani Geita yaililia serikali.

14 April 2021
Share

Shule ya Sekondari Magema iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani Geita ina walimu wawili tu hali inayopelekea idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufundishwa masomo mengine yakiwemo ya sayansi  kutokana na uhaba wa walimu hali inayotishia kushuka kwa ufaulu katika mitihani yao.


Wakizungumza na ITV wanafunzi katika shule hiyo wameiomba serikali kuwaongezea walimu kutokana na walimu wawili waliopo kutokidhi kufundisha masomo yote.


Aidha, Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wazazi na wanafunzi juu ya changamoto hiyo amesema serikali imeanza kuchukua hatua huku akiwataka wazazi kukomesha utoro kwa watoto wao.