Back to top

SIDO mkoani Kigoma yazindua mashine mpya ya kuchakata zao la muhogo

05 December 2018
Share

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini SIDO mkoani Kigoma limezindua mashine mpya ya kusindika mazao mbalimbali  ikiwemo zao la muhogo, teknolojia itakayowasaidia wakulima kuondokana na umaskini kwa kukosa zana bora za kusindika muhogo na kulazimika kuuza mazao ghafi kwa bei ndogo.
  
Meneja wa SIDO mkoa wa Kigoma Gervas Ntahamba amesema shirika hilo limekuwa likibuni teknolojia mbalimbali za kuwasaidia wakulima ili waweze kutumia teknolojia ambazo zitasaidia kuondoa changamoto ya kuuza mazao ambayo hayakuchakatwa.
 
Kwa upande wake meneja wa kituo cha teknolojia SIDO mkoa wa Kigoma Mabamba Majogoro amesema mashine hizo mpya zinauwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuchakata kilo 750 za muhogo kwa saa.