Back to top

Simba waliovamia makazi ya watu wazua hofu mkoani Geita.

18 October 2018
Share

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Shantamine  ya mjini Geita wameshindwa kuendelea na masomo huku wazazi wakiacha kufanya kazi za maendeleo kwa kuhofia usalama wa maisha yao baada ya kuibuka kwa kundi la wanyama pori aina ya Simba kuvamia vijiji vya kata ya Bungi,Hwangoko na kata ya Mgusu hali iliyosababisha hofu kubwa kwa jamii.

Hayo yamebainisha na mbunge wa jimbo la Geita kwa niaba ya wananchi Mhe.Costantine Kanyasu wakati akizungumza na ITV na amesema kuwa taarifa za wanyama hao zimesababisha hofu kubwa kwa wananchi huku wanafunzi na walimu wakiiomba serikali kudhibiti wanyama wakali kwenye makazi ya watu.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Geita ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Josephat Maganga amekiri kupokea taarifa hizo na kusema ofisi yake imeleta wataalamu na askari wanyama pori kutoka maliasili ambao kwa sasa wapo msituni wakifuatilia nyendo za wanyama hao.