Back to top

Simbachawene:Mwamposa alijaribu kutoroka baada ya tukio la Moshi.

02 February 2020
Share

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe George Simbachawene amesema Jeshi la polisi linamshikilia mtume na nabii Boniface Mwamposa baada ya kutoroka mjini Moshi kufuatia vifo vya watu 20 na majeruhi 16 ambao walikuwa wanakanyaga mafuta ambapo mchungaji huyo amekamatwa Dar es salaam.

Akizungumzia tukio hilo lilotokea Februari Mosi mwaka huu Waziri Simbachawene amesema  kuna kila sababu ya kuchukua hatua stahiki kwa mchungaji huyo.

Aidha Waziri Simbachawene amewataka viongozi wote wa madhehebu ya dini hapa nchini wanapofanya mikusanyiko ya watu kuhakikisha wanaimarisha usalama wa watu ambapo amesema mchungaji huyo pia alikiuka sheria kutokana na kibali alichopewa.

Wakati huo Waziri Kivuli wa mambo ya ndani ya nchi Mhe Godbless Lema amesema tukio hilo ni la kusikitisha huku akisema kuwa ni uzembe wa Jeshi la polisi kushindwa kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.