Back to top

Sita wajeruhiwa na fisi Shinyanga, inadaiwa walimzingira ili wamuue.

28 March 2020
Share

Watu sita wa familia moja wakazi wa kijiji cha mwangalanga kata ya Samuye wilayani Shinyanga wamejeruhiwa kwa kung’atwa na fisi katika maeneo mbalimbali ya miili yao na ikidaiwa watu hao wamejeruhiwa na fisi huyo baada ya kumzingira kwa lengo la kumuua .

Hata hivyo majeruhi watano kati ya hao hali zao zinaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitali na kutibiwa hatimaye kuruhusiwa huku majeruhi mmoja ambaye ni Zengo Jitonjwa miaka 56 ambaye alijeruhiwa na fisi huyo mikononi na mdomoni bado hali yake sio nzuri na anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia leo na kueleza kuwa fisi huyo ameshauawa na wananchi kwakuwa alivamia maeneo ya makazi.