Back to top

Spika wa Bunge Mh Job Ndugai ameongoza wabunge kupima VVU.

21 June 2018
Share

Spika wa Bunge Mh Job Ndugai ameongoza wabunge kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika viwanja vya Bunge ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya furaha yangu iliyozinduliwa na Mh Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa June 19 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kupima Spika Ndugai amewahamasisha waheshimiwa wabunge na wananchi kwa ujumla hasa wanaume ambao takwimu zinaonyesha wako nyuma katika kupimaji VVU ili kutambua afya zao na kuishi kwa amani kwani hata ukikundulika kuwa na virusi vya ukimwi si mwisho wa maisha

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera Ajira na watu wenye ulemavu Mh Jenister Mhagama amesema wameamua kuwashirikisha waheshimiwa wa Bunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi ili kuonesha kwamba kupima ni jambo la kawaida

Kampeni ya ‘Furaha yangu,pima jitambue,ishi’ ilizinduliwa June 19 lengo likiwa kuhamasisha upimaji wa VVU na matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ARVS mapema katika mapambano ya ugonjwa wa ukimwi.