Back to top

SUMATRA yatoa onyo kwa mabasi ambayo hayajafungwa vidhibiti mwendo

19 October 2018
Share

Mamlaka ya udhibiti wa usafirishaji wa majini na nchi kavu (SUMATRA) imepiga marufuku Mabasi ambayo yatakuwa hayajafunga vifaa vya udhibiti mwendo kuingia barabarani hadi watakapokamilisha zoezi hilo linalolenga kumaliza ajali za barabarani.
 
Akizungumza na ITV katika zoezi la kufunga vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na vifaa vya kutoa taarifa za matukio ya barabarani yakiwemo ya utekaji wa magari, afisa mfawidhi  SUMATRA mkoa wa Tabora Bw. Joseph Michael amesema kuwa zoezi hilo ni la muda wa juma moja na baadae msako unafuata.

Mtaalamu wa kufunga vifaa hivyo Bw.Ramadhani Ndijue amesema kuwa, pamoja na kufungwa kwa vifaa hivyo wanaongezewa pia kifaa cha kutoa taarifa kama gari hilo limepata ajali au limetekwa na majambazi na dereva kutoa taarifa bila ya waarifu kujua.