Back to top

SUMATRA yatoa saruji mifuko 30 kuboresha miundombinu ya elimu.

04 November 2018
Share

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na majini imetoa saruji tani 30 yenye thamani ya Shilingi Milioni tisa na laki tano kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu na huduma za afya.

Miradi hiyo ni pamoja na kujenga vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za watumishi katika halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi.

Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkurugenzi Mkuu wa  mamlaka hiyo, Bwana Gilliard Ngewe amesema wameguswa na matatizo yanayoikabili sekta hizo na hivyo kuamua kuchangia ili kuboresha hali ya shule za msingi pamoja na kuboresha huduma katika zahanati za wilaya hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bwana Amos Makala amesema serikali pekee haiwezi kukabiliana na matatizo yote na kuomba wadau wengine kujitokeza katika kuchangia kupunguza shida zilizopo.