Back to top

TAA yakanusha taarifa za abiria kuibiwa pochi katika eneo la ukaguzi.

13 September 2018
Share

Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini(TAA) yakanusha taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa abiria Awapef Akrabu anayedai kuibiwa pochi yake katika eneo la ukaguzi wa abiria Katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 8 mwaka huu kuwa sio za kweli.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo  Mkuu Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Richard Mayongela  alionyesha picha za mnato za CCTV ambazo zilimuonyesha abiria huyo akiwa katika eneo linalodaiwa kuhusika na upotevu wa pochi hiyo.

Bw. Awali Akrabu ni mmoja wa ndugu wa abiria huyo ambaye alikuwepo katika mkutano kati ya  waandishi wa habari na TAA anasema ameziona picha zinazomuonyesha ndugu yao lakini hawezi kusema lolote.