Shirika linaloshughulika na mazingira na maendeleo (MCDI) kwa ufadhili wa shirika la mazingira duniani( WWF) linapambana kuokoa miti iliyo hatarini kupotea ukiwemo wa mnungunungu ambao wananchi wamekuwa wakitumia majani yake kwa tiba.
Akizungumza katika mahojiano na ITV Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanamazingira Afisa wa shirika la MCDI Bw. Kassim Ulega anasema ili kuuokoa mti huo wameanza kuotesha miche ya mnungunungu katika kijiji cha Mchakama mkoani Lindi.