Back to top

Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa sheria zatakiwa kuongeza ufanisi.

29 November 2020
Share

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof.Ibrahim Hamis Juma amezitaka taaasisi mbalimbali nchini zinazosimamia utekelezaji wa sheria na kutetea haki za binadamu kuongeza ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma, hasa maeneo ya vijijini.

Jaji Mkuu ametoa maelekezo hayo kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Wanasheria wanawake Jijini Dar es Salaam.

Amesema upatikanaji wa huduma za sheria kwenye maeneo ya vijijini bado ni mdogo lakini watu wengi wanaoishi maeneo hayo wanahitaji  utatuzi wa sheria kutokana na migorogoro mbalimbali ikiwemo ya familia, mirathi, pamoja na watu kudhulumiwa haki zao.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini, Bi.Lulu Mwanakilala pamoja na kuelezea mafanikio ya kutetea haki za wanawake na watoto katika kipindi cha miaka 30 ya taasisi hiyo, amesema jamii bado ina kila sababu ya kupatiwa elimu ya kupinga unyanyasaji wa jinsia kwa wanawake na watoto ili haki iendelee kuwepo.