Back to top

TAKUKURU imeiomba Mahakama kumchukua aliyekuwa Rais wa TFF.

16 January 2019
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam  kumchukua aliyekuwa Rais wa (TFF) Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ili kwenda kuwahoji.
 
Maombi hayo, yamewasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka lakini wakili Swai ameieleza mahakama kuwa mashahidi waliotarajiwa kufika leo wamepata udhuru, ambapo mmoja anaumwa na mwingine amepangiwa kazi Utumishi.
 
Aidha Swai ameiomba mahakama hiyo amchukue Malinzi na Mwesigwa kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano Takukuru kwa sababu kuna vitu wanataka kuviongezea
 
Kufuatia hayo, upande wa utetezi wameiomba mahakama ichukulie suala hilo kwa uzito kwa sababu washtakiwa wapo ndani wanateseka 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi January 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.