Back to top

TAKUKURU Geita yawakamata vigogo watatu wa serikali kwa rushwa.

15 July 2020
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita inawashikilia watuhumiwa watatu akiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya Famoyo,Mhandisi wa Maji Halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwa tuhuma za kushawishi na kupokea milioni mia nne kuhujumu mradi wa maji wa Nyamtukuza

ITV ilifika ofisi za TAKUKURU mkoa wa Geita na kushuhudia watuhumiwa hao wakiwa chini ya ulinzi wa Kamanda TAKUKURU mkoa wa Geita Leonidas Felix.

Kamanda huyo wa TAKUKURU anasema taasisi hiyo inaendelea kumsaka mshauri wa mradi huo anayedaiwa kuwakimbia maafisa wa TAKUKURU ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa waliokamatwa ili kufikishwa mahakamani.