Back to top

Takukuru Iringa yabaini miradi ya maji kujengwa chini ya kiwango.

20 January 2019
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imebaini utekelezaji wa chini ya kiwango katika ujenzi wa miradi minne ya maji yenye dhamani ya zaidi ya shingi bilioni mbili na milioni miatano

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha mwezi oktoba hadi Desemba mwaka jana Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Iringa Bwana Mweli Kilimali amesema uchunguzi wa kina kuhusu ubadhrifu wa miradi hiyo unaendelea kwa hatua zaidi za kisheria.

Ameitaja miradi hiyo ambayo ipo chini ya kiwango kuwa ni mradi wa umwagiliaji wa kijiji cha Idodi uliojengwa kupitia mpango wa BRN na mradi wa maji safi na usafi wa mazingira kwa vijiji vya Migori na Mtera.

Miradi mingine ni ukarabati wa mradi wa maji wa kijiji cha Magubike na mradi wa usafi wa mazingira kwa vijiji vya Izazi na Mnadani.

Bwana Kilimali amesema mradi wa maji safi na usafi wa mazingir kwa vijiji vya Migori na Mtera unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya GNMS kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni 385 ambapo mradi wa majisafi na usafi wa mazingira kwa vijiji vya Izazi na Mnadani unajengwa na kampuni ya Lekashingo Building Costruction kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 855.