Back to top

TAKUKURU yaagizwa kuwabana walarushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

21 June 2020
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amesema Serikali imewaagiza Makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini wahakikishe wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Lindi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea akiwa njiani kwenda Wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu amesema kitendo cha kutoa na kupokea rushwa ni kosa, hivyo viongozi hao wa (TAKUKURU) nchini hawana budi kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Waziri Mkuu pia amewataka Makamanda wa (TAKUKURU) katika wilaya zote nchini wahakikishe wanawakamata watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakiwemo na wapambe ambao ndio wachochezi wa vitendo hivyo.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki, hivyo kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa.