Back to top

TAKUKURU yabaini mianya ya rushwa kwenye usafirishaji zao la Korosho.

11 October 2018
Share

Utafiti uliyofanywa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Ruvuma umebaini uwepo mkubwa wa mianya ya rushwa katika ukusanyaji na usafirishaji wa zao la Korosho.

Akizungumza katika kikao kazi na wadau wa Korosho katika mikoa iliyofanyiwa utafiti amesema juhudi za makusudi zinaitajika ili kukabiliaana na mianya hiyo ambayo Inagusa maeneo mengi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya Korosho nchini Prof.Wakuru Magigi amesema kwenye tasnia ya Korosho kuna upotevu mkubwa wa korosho za wananchi hasa pale korosho zinapotoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye maghala makuu na kuomba TAKUKURU kusaidia maeneo haya.

Hata hivyo wadau wa Korosho wametaka kuona changamoto za upotevu wa fedha na korosho za wakulima katika msimu huu 2018/2019 zinashughulikiwa ili mkulima aweze kufurahia jasho lake.