Back to top

TAKUKURU yamtia mbaroni Mfanyakazi wa TAZARA kwa tuhuma za rushwa.

14 February 2019
Share

Mfanyakazi wa shirika la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bahati Selemani amekamatwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, (TAKUKURU), mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki mbili kutoka kwa mfugaji mmoja wilayani Mbarali.

Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya, Julieth Godfrey Matechi amesema mtuhumiwa amekamatwa baada ya kuomba rushwa ya shilingi 400,000 kutoka kwa mfugaji aliyekuwa akilisha ng'ombe yake kwenye hifadhi ya reli katika kijiji cha Chimala wilayani Mbarali ili asimchukulie hatua za kisheria na TAKUKURU imemkamata wakati akipokea rushwa ya shilingi 200,000 ambazo ni sehemu ya shilingi 400,000 alizoziomba.