Back to top

Tanzania imebakiwa na benki za wananchi 4 nchi nzima-BOT

16 September 2019
Share

Benki kuu ya Tanzania (BOT) imesema Tanzania imebakiwa na benki za wananchi nne tu ambazo zinafanyakazi nchi nzima baada ya  benki nyingi zilizokuwa zinafanyakazi  kufa  kwa kushindwa kujiendesha kutokana na  kukosa mitaji.

Mkurugenzi Mkuu Benki kuu ya Tanzania Bw.Jerry Sabi ameyasema hayo wilayani Mwanga wakati akizungumza na wanahisa wa benki ya wananchi Mwanga ambayo imepandishwa hadhi na kuwa benki ya kibiashara.

Amesema benki nyingi nchini zinakufa kutokana na kukosekana kwa utawala bora baina ya wasimamzi kutokana na watendaji kula njama na wanachama kushiriki  kuchukua mikopo mikubwa ambayo wanashindwa kuirejesha na kugawana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Benki ya wananchi Mwanga Bw.Ridhuani Ringo amesema hali ya benki hiyo kwa sasa inaridhisha baada ya kubaini sababu zilziokuwa zinapelekea benki kufa  na kuchukua hatua na kwamba kwa sasa benki hiyo inakidhi masharti ya benki kuu ya kuwa na kiasi cha shilingi bilioni 5 ili iweze kuwa benki ya kibiashara nchni Tanzania.