Back to top

Tanzania inaongoza kuwa na idadi kubwa ya Simba wapatao elfu 20.

17 October 2020
Share

Tanzania inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya SIMBA wapatao elfu 20 ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya SIMBA walioko duniani ambao wamekuwa na mvuto kwa wageni wengi wanaoitembelea Tanzania wakiwemo wawindaji wa kitalii.

Hayo yamesemwa na Naibu Kamishina, Utalii na Biashara kutoka mamlaka ya wanyamapori Tanzania (TAWA) alipokutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa klabu kubwa ya uwindaji wa kitalii duniani iitwayo The Safari Club International ya nchini Marekani ambayo imeitaja Tanzania kuwa nchi bora kabisa duniani kwa uwindaji wa kitalii ulimweguni.

Amezungumzia kuhusu upekee wa shughuli za uwindaji wa kitalii nchini Tanzania ikiwemo amani na utuvu mambo ambayo yanawafanya wageni kutoka mataifa mbalimbali kupenda kuitembelea Tanzania.

Naye rais mstaafu wa klabu hiyo ya uwindaji wa kitalii duniani Steve Skold amesema klabu hiyo yenye matawi zaidi ya 300 na wanachama zaidi ya 50,000 kutoka nchi mbalimbali duniani itaendelea kuiheshimu tanzania nchi ambayo ina wanyamapori wengi ambao wanafaa kwa uwindaji wa kitalii ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.