Back to top

Tanzania kinara mapambano dhidi ya rushwa,ni ya kwanza kati ya nchi 35

09 August 2019
Share

Tanzania imekuwa ya kwanza kati ya nchi 35 za Afrika katika kipengele cha juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2019 ikifuatiwa na nchi za Lesotho na Sierra leone.

Yameainishwa katika taarifa ya utafiti wa kupima hali ya rushwa iliyotolewa Julai 11 mwaka huu na taasisi za kimataifa zinazofanya tafiti za Transparency International na Afro Barometer inayoitwa Global Corruption barometer Africa 2019.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Diwani Athumani ambapo amesema katika taarifa hiyo Tanzania imefanya vizuri katika maeneo mawili kwanza utendaji mzuri wa serikali ya awamu ya tano na katika eneo la pili ni katika kukuza imani kwa wananchi dhidi ya serikali yao kutokana na jitihada ya kupambana na matukio ya rushwa.