Back to top

Tanzania kuendelea kutunza maporomoko ya Kihansi yenye vyura.

21 August 2019
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.George Simbachawene amesema serikali ya Tanzania itaendelea kutunza maporomoko ya Kihansi yenye vyura wa kipekee duniani wanaopatikana hapa nchini ambao pia wana uwezo wa kuzaa.

Mhe.Simbachawene ameyasema hayo katika maporomoko ya Kihansi wilaya ya Kilombelo mkoani Morogoro baada ya kupanda milima hiyo na kuona namna ya utunzaji wa vyura hao wanaopatikana Tanzania pekee.

Amewataka wataalamu kuendelea kufanya utafiti ili nchi iweze kuwa na vitu vingi na muhimu vitakavyosaidia kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake mkurugenzi wa baraza la usimamizi wa mazingira NEMC Dkt.Samweli Gwamaka amesema wao ni watekelezaji wa sheria na wataendelea kuzisimamia katika uhifadhi, huku mkurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira Prof.William Mwigoa pamoja na mambo mengine akisema wao kama serikali wanasimamia mkataba ambao serikali imesaini wa kutunza bayonai na urithi unaopatikana katika viumbe hai vya nchi.