Back to top

Tanzania yagundua uwepo wa aina saba adimu ya samaki nchini.

13 September 2018
Share

Tanzania imegundua uwepo wa aina saba adimu ya samaki nchini ambao hawapatikani mahali pengine popote duniani, ambapo samaki hao hupatikana kwenye mabonde na maziwa mbalimbali kufuatia utafiti uliofanywa kwa muda wa miaka mitano kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt.Hamisi Nikuli kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Dkt.Rashid Tamatamah ameyasema hayo katika mkutano wa kutoa ripoti ya tathmini ya samaki wanaopatikana hapa nchini ambapo alisema ni dhamana ya kila mmoja wetu kulinda viumbe hivi visitoweke kwaajili ya vizazi vijavyo.

Naye Mtafiti Dkt.Benjamin Ngatunga ametaka zitumike njia mbadala za kuondokana na uvuvi haramu kwa kutumia njia ya ufugaji samaki kwa wingi huku samaki aina ya Sato akitajwa kuwa samaki anayefaa kufugwa na kupendekeza kuwe na mahali pakuzalishia samaki ili vifaranga bora vipatikane.