Back to top

Tanzania yashika nafasi ya 14 kwa uwajibikaji na utawala bora Afrika.

04 December 2018
Share

Tanzania imeshika nafasi ya 14 kati ya nchi 54 zinazoongoza kwa uwajibikaji na utawala bora barani Afrika kutokana na serikali kuboresha mfumo wa utawala unaozingatia uwazi, haki za binadamu, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi pamoja na urahisi kwa kufanya biashara na uwekezaji.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya Mo Ibrahim ambayo hutoa ripoti kila mwaka juu ya serikali zenye uwajibikaji na utawala bora barani Afrika ambapo Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 17 iliyoshika mwaka jana.