Back to top

TASAF Yatoa milioni 72 kusaidia miundombinu ya shule ya msingi Kongo.

12 July 2018
Share

Miundombinu  ya shule ya msingi kongo iliyopo wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi imeboreka baada ya  mfuko  wa maendeleo ya jamii TASAF awamu ya tatu kutoa shilingi milioni 72 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, vyoo, miundombinu ya maji pamoja na kuweka Sola.

Kauli hiyo imetolewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Betila Mapua baada ya  kutembelewa   na waandishi wa habari  kujionea miradi ya TASAF iliyotekelezwa katika shule hiyo.

Amesema uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo umesaidia kuondoa changamoto ikiwemo kuongeza matundu ya vyoo vya wanafunzi pamoja na ujenzi wa choo cha walimu ambao hapo awali walikuwa wanalazimika kujisaidia na vichakani na hivyo kuatarisha maisha yao.

Hata hivyo amesema kwa sasa shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa ofisi za walimu pamoja na nyumba za walimu hivyo ameomba jamii kuendelea kuisadia ili iweze kukamilisha miundombinu hiyo.

Kwa upande wake mratibu wa TASAF wilaya ya Nachingwea James Mbakile amesema katika kusaidia changamoto za shule hiyo TASAF imetoa shilingi milioni 72  lengo likiwa kuboresha mazingira ya shuele ili wanafunzi wapate elimu bora.

Mbali na ukarabati huo fedha hizo pia zimetumika kuweka sola, na  miundombinu ya maji.