Back to top

TBA yatoa siku 30 kwa wapangaji sugu kulipa pango.

27 November 2020
Share

Wakala wa majengo mkoani Mtwara imetoa siku 30 kwa wateja sugu kulipa pango za nyumba za wakala huo kabla ya hatua za kuwaondoa hazijachukuliwa.

Agizo hilo limetolewa na kaimu meneja wa wakalawa majengo mkoani Mtwara Edward Mwangasa amesema zoezi la kuwaondoa wapangaji sugu litafanyika baada ya siku 30 kwisha hivyo amewataka wadaiwa hao kulipa fedha hizo kabla ya muda huo kumalizika.

Amesema tayari jeshi la polisi linataarifa hiyo na limejiandaa kuwaondoa na kusisitiza pamoja na kuondolewa kwenye nyumba hizo watalazimika kulipa fedha hizo kwa mujibu wa taratibu za upangaji wa nyumba hizo.

Kwa upande wake msimamizi wa mali za wakala Mtwara Manase Mkumbo amesema baadhi yawapangaji wamekuwa wakilimbikiza pango za nyumba na hivyo mwisho wake kushindwa  kulipa pango kwa muda unaotakiwa.

Hata hivyo baadhi ya wapangaji wamekiri kuchelewesha kulipa pango na hivyo kuadi kulipa kabla ya muda uliopangwa kwisha.