Back to top

TCB imesema Tanzania inazalisha kahawa tani elfu 50 kwa mwaka.

29 September 2020
Share

Bodi ya kahawa nchini (TCB) imesema Tanzania inazalisha kahawa tani elfu 50 kwa mwaka ambapo asilimia 93 ya kahawa hiyo husafirishwa kuuzwa masoko ya nje ya nchi.

Kaimu mkurugenzi wa ubora na uhamasishaji wa kahawa bodi ya kahawa nchini Bw.Primus Kimario amesema Watanzani hutumia asilimia saba tuu ya kahawa inayozalishwa hapa nchini.

Amesema kutokana na changamoto hiyo bodi ya kahawa imeanzisha utaratibu wa uhamasishaji wa unywaji wa kahawa hapa nchini ambapo zaidi ya wadau 84 walioko kwenye mnyororo wa thamani kwa kuhudhuria maadhimisho ya wiki ya unywaji wa kahawa ambao unatarajia kufanyika mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wa baadhi ya wanywaji wa kahawa mkoani Kilimanjaro wamesema kuna haja ya ya Watanzania kuhamasishwa zaidi kupenda kutumia kahawa inayozalishwa hapa nchini ikiwa na pamoja na kuhamasisha vijana kujihusisha kwenye shughuli za uzalishaji wa kahawa.

Bodi ya kahawa mwaka huu itaadhimisha siku ya unywaji wa kahawa dunia ambapo kitaifa itafanyika mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya Uhuru Park mjini Moshi na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.