Back to top

TCRA kuchunguza kampuni za simu zinazowadhulumu watumiaji wake.

24 February 2020
Share

Serikali imetoa wiki mbili kwa Mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA kuzichunguza na kuzichukulia hatua stahiki baadhi ya kampuni za mitandao ya simu ya mkononi zinazoshutumiwa na wananchi kwa kukata ovyo vifurushi na wakiweka hela zinakwisha kabla ya muda wa matumizi .

Naibu Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ametoa kauli hiyo mara baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya simu ya Tigo katika kijiji cha Mavuji kata ya Mandawa wilayani Kilwa mkoani Lindi kufuatia malalamiko mengi aliyoyapokea kutoka kwa wananchi.