Back to top

TCRA Kurudisha vifurushi kama ilivyokuwa awali.

14 April 2021
Share

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabir Bakari Kuwe amesema  wanashughulikia suala la vifurushi ili virudi kama ilivyokuwa awali.
.
"Kama ambavyo maelekezo ya Serikali yametolewa tunafuatilia kwa karibu sana suala la mabando au vifurushi ili virudi kama ilivyokuwa awali”
Akaongeza kuwa" Tuna-monitor na tunategemea muda si mrefu vitakamilika na vitarudi vyote kama ilivyokuwa awali, tunafuatilia kila saa na muda sio mwingi vitarudi kama zamani, maelekezo ni kwamba tunarudisha mabando yote kama mwanzo".