Back to top

TCRA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kulipia masafa yao.

20 June 2018
Share

Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA ) imewataka Wamiliki wa vyombo vya habari na  Mitandao ya Kijamii kuzingatia sheria na kanuni mpya  za maudhui zinazolenga kuongeza ufanisi katika ukuaji wa teknolojia ya upashanaji wa habari zenye mwelekeo wa kukuza uchumi unaoenda sambamba na sera ya serikali ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini,Mhandisi James kilaba ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa mawasiliano mkoani Mwanza kilicholenga kuwakumbusha sheria na kanuni mpya zilizotolewa mapema mwaka huu na kuanza kutumika mwezi Machi zikiwemo za mitandao ya kijamii na wamiliki wa vyombo vya habari ambao hawajalipia masafa kuhakikisha wanalipa kabla ya Juni 30 mwaka huu.