Back to top

TCU imekifutia usajili kituo cha chuo kikuu kishirikishi Moshi.

09 November 2018
Share

Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imekifutia usajili kituo cha chuo kikuu kishirikishi cha kumbukumbu ya Stefano Moshi na kufungia programu 9 za shahada ya kwanza kwa vyuo vikuu vinne.

Hayo yamesemwa na Prof.Charles Kihampa-Katibu Mtendaji TCU ambapo TCU pia imewahamisha wanafunzi wanaoendelea na masomo, na kusitisha udahili wa wanafunzi wapya katika baadhi ya vyuo vikuu nchini.

Kusitishwa udahili wa wanafunzi wapya katika vyuo hivyo kunafuatia jumla ya vyuo vikuu vilivyositishwa udahili kwa mwaka wa masomo 2018/19 kufikia 12.

wanafunzi waliohitimu masomo kwa mwaka 2017/18 watatunukiwa tuzo za katika vyuo walivyosoma na  uamuzi huu uliotolewa na TCU hautowaathiri wao.