Back to top

Tenki la mafuta lajeruhi mmoja Kahama.

09 August 2020
Share

Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika amenusurika kifo baada ya upande wa nyuma wa tenki la mafuta lililokuwa linachomelewa katika eneo la Bijampola mjini Kahama kufyatuka kama mlipuko na kusababisha madhara katika nyumba mbili zilizokuwa jirani.

Majeruhi huyo amekimbizwa katika hospitali ya halmashauri ya mji Kahama kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba amethibitisha kupokea kwa tukio hilo.